Ibada za Kanisa Katoliki zimefutwa kwa wiki ya pili katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo, serikali imesema ni kutokana na uwezekano wa kutokea mashambulizi zaidi kutoka kwa kundi lenye mafungamano na Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS ambalo limehusishwa na mashambulio ya mabomu wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Padri Edmund Tillakaratne, msemaji wa Parokia ya Colombo, amesema Kardinali Malcolm Ranjith amefuta ibada zote za Jumapili katika jimbo hilo kulingana na ripoti za usalama za hivi karibuni.
Waziri mmoja wa Sri Lanka amesema mawaziri wa serikali wanaweza kulengwa katika mashambulizi ya kigaidi. Wakati huo huo Polisi nchini humo jana jioni walichapisha majina na picha za watu tisa wanotuhumiwa kuhusika na mashambulio ya siku ya Pasaka kwenye makanisa na hoteli za kitalii yaliyosababisha kuawa watu wapatao 253.
Related Posts
Rais Dk. Shein asisitiza wafanyakazi wa umma kufanya kazi katika mazingira mazuri
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa miongoni[...]
May 02, 2019Wasanii Afrika Mashariki Waomboleza Msiba wa Mengi
Kundi la wasanii wa muziki kutoka nchini Kenya Sauti Sol, limeungana na Afrika nzima kuombeleza msi[...]
May 02, 2019Jeshi la Polisi Lafunguka Kuhusu Kutangaza Nafasi za Ajira
Jeshi la Polisi limesema kuwa halijatangaza nafasi za ajira katika chombo chochote cha habar[...]
May 02, 2019Freeman Mbowe amlilia Dkt.Reginald Mengi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salamu pole kufuat[...]
May 02, 2019Kikosi cha Yanga SC kitakachocheza na Tanzania Prisons leo
Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) kuendelea tena leo ambapo Yanga SC watacheza dhidi ya Tanzania Pr[...]
May 02, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.