Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona kwamba watumishi wa umma wanafanya kazi zao wakiwa katika mazingira yaliyo bora na salama zaidi.
Dk. Shein aliayasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi za Serikali huko Gombani Chake Chake Pemba, Mkoa wa Kusini Pemba, ambapo viongozi mbali mbali wa vyama na serikali pamoja na wananchi na wafanyakazi walihudhuria.
Rais Dk. Shein alisema kuwa uzinduzi wa jengo hilo ni miongoni mwa vielelezo muhimu vya utekelezaji wa lengo hilo kwani majengo ya ofisi ndio mahali pa kufanyia kazi ambapo hutumia muda mwingi ambayo ni theluthi moja ya siku nzima baada ya kutoka nyumbani.
Alieleza kuwa kuwa na mahala pazuri pa kufanyia kazi kunampelekea mtendaji afanye kazi kwa furaha, umakini na kujiamini Zaidi na ndio maana Serikali imeamua kujenga.
Aliongeza kuwa ujenzi wa jengo hilo ni jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia maamuzi ya Baraza la Mapinduzi ambapo hatua yote hiyo ni kuwawwzesha wafanyakazi katika mazingira mazuri.
Alieleza kuwa ujenzi huo unatokana na baadhi ya ofisi kuchakaa, nyengine hazina nafasi ya kutosha kwa ajili ya watumishi pamoja na wananchi wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma.
Hata hivyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa baadhi ya Wizara na Taasisi nyengine za Serikali zililazimika kukodi nyumba kutokana na uhaba wa majengo halisi ya kiofisi hali ambayo haipendezi hivyo Serikali itaendelea kujenga majengo ya Ofisi Unguja na Pemba.
Rais Dk. Shein alisema kuwa Serikali imejenga ofisi hizo ili kurahisisha utoaji wa huduma hivyo, kila mfanyakazi ahakikishe kwamba anawajibika ipasavyo kulingana na dhamana na majukumu ya kazi aliyopangiwa.
Hivyo, aliwataka wafanyakazi wahakikishe wanatumia vizuri muda wa kazi kwa kufanya mambo yanayopaswa kufanywa katika sehemu za kazi.
Alisema kuwa Serikali itaongeza mshahara kwa kima cha chini na juupale mapato yatakapoongezeka kwa wafanyakazi kuzidi kujituma na kuendelea kufanya kazi kwa ari, taratibu na nidhamu za kazi
Next
This is the most recent post.
Previous
Ibada za Kanisa Katoliki Zafutwa kwa Wiki Mbili
Related Posts
Ibada za Kanisa Katoliki Zafutwa kwa Wiki Mbili
Ibada za Kanisa Katoliki zimefutwa kwa wiki ya pili katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo, serikali[...]
May 02, 2019Wasanii Afrika Mashariki Waomboleza Msiba wa Mengi
Kundi la wasanii wa muziki kutoka nchini Kenya Sauti Sol, limeungana na Afrika nzima kuombeleza msi[...]
May 02, 2019Jeshi la Polisi Lafunguka Kuhusu Kutangaza Nafasi za Ajira
Jeshi la Polisi limesema kuwa halijatangaza nafasi za ajira katika chombo chochote cha habar[...]
May 02, 2019Freeman Mbowe amlilia Dkt.Reginald Mengi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salamu pole kufuat[...]
May 02, 2019Kikosi cha Yanga SC kitakachocheza na Tanzania Prisons leo
Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) kuendelea tena leo ambapo Yanga SC watacheza dhidi ya Tanzania Pr[...]
May 02, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.