Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (Cuf), haukuwa wa ghafla bali ulikuwa na mchakato.
Akizungumza katika kipindi maalumu cha Kwanza TV, wakati akihojiwa na Maria Sarungi, leo Jumatano Machi 20, Zitto amesema pamoja na kwamba ilikuwa ni mchakato wa maandalizi wa kwao (kina Maalim Seif) na wao (ACT) walijiandaa kwa lolote, kwani kwa muda mrefu walikuwa wanasisitiza katiba ifuatwe.
“Watu wasidhani mambo haya ni maandalizi ya muda mchache baada ya hukumu, bali ni maandalizi ya muda mrefu ya kujenga imani kujiandaa kisaikolojia na si ACT pekee bali vyama vyote na watu wanaopenda mabadiliko na wamechoshwa na kuburuzwa ndani ya CCM.
“Ilikuwa Maalim akoseshwe jukwaa ili ashindwe… Ni lazima juhudi za mapambano ya kudai demokrasia ziendelee na kuungana na wenzetu ambao hawakutendewa haki ili waweze kuendelea na mapambano,” amesema Zitto.
Post a Comment