0
Ndoa ya Shamsa Ford Kuvunjika Kisa Mtoto?
Msanii wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amewajibu watu wanaomsema kwamba ameshindwa kumzalia mume wake Chid Mapenzi mtoto na kusema  kwamba ndoa si mtoto na kila mtu ana mipango yake ya kuzaa baada ya ndoa, hivyo waache kuongea wasiyoyajua.

Akiongea na eNewz , Shamsa amesema kila ndoa ina mipango haswa katika suala la kupata mtoto kuna wengine wanapanga kuzaa hata baada ya miaka mitano hivyo hata yeye na mume wake wana mipango yao ya ndani ya ndoa hivyo pale mwenyezi mungu atakapowabariki watapata mtoto.

"Kikubwa ambacho naweza kuwaambia watu ni kwamba tuombeane mema kwa kuwa maisha ni mafupi na hakuna anayeujua mwisho wake na hata katika dini Mungu amesema kwamba ukimuombea mwezio mema na wewe utabarikiwa zaidi", amesema Shamsa.

"Hivyo kama kuna mtu ambaye hajaolewa na ananiombea mimi niachane na mume wangu basi ni bora awe makini kwa kuwa yeye anaweza akakosa hata mume wa kumuoa kwa kuniombea mimi mabaya", ameongeza.

Shamsa awazungumzia waliomsema siku ya harusi

Hata hivyo Shamsa alimalizia kwa kusema kwamba siku ya harusi yao kuna watu walidhani kwamba ataachana na Chid baada ya muda mfupi lakini kwa uwezo wa Mungu mpaka sasa ni mwaka wa tatu na bado wapo pamoja hivyo anaamini kwamba talaka si jambo jema kidini hivyo Mungu hawezi ruhusu ndoa yao ivunjike  na kama ikivunjika basi anaamini itakuwa ni mipango ya Mungu.

Post a Comment

 
Top