Mwigizaji wa filamu Bongo, Muna Love amewashangaa baadhi ya watu wanaojadili picha zake kwenye mitandao kutokana na kuonekana kung'aa sana.
Muna aliyepata umaarufu kwenye mtandao wa kijamii wa Instgram amekuwa akiongenana aking'aa zaidi lakini ameeleza hilo linatokana na kuwa karibu na Mungu.
"Watu walishazoea siku zote mtu akiwa ameokoka anakuwa hapendezi anakuwa tofauti wakati kwa Mungu kuna kila ambacho unakihitaji, kuna kila kitu ambacho unamwomba wewe atakupatia kwa sababu umemwambini na kumpa maisha yako, nimemwamini na kumpa maisha yangu Mungu anaangalia moyo wangu haangalii kuwa nimevaa hivi," amesema Muna Love.
Ameendelea kwa kusema, 'Yeye ndiye anayenibariki na kuniongoza kwahiyo hata kupendeza kwangu kunatokana na kung’arishwa na Mungu, angekuwa haning’arisha nisingependeza, kwani wangapi wanapendeza na kuvaa nina kitu gani cha ajabu mpaka kikamshtua mtu, hiyo picha ni ya kawaida sana lakini kwa sababu Mungu ndio maana wanaiona ya tofauti'.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment