0

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda na watumishi wengine 12, kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh bilioni 5, kutokana na hasara kwenye ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi mkoani humo.

Agizo hilo la Mkuu wa Mkoa limekuja kufutia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kusema ujenzi huo haukufuata taratibu za manunuzi na Kwamba hata mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi huo hakuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo jambo ambalo limeipelekea serikali hasara.

Aidha katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole sendeka ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahusika wote waliokimbia katika kikao cha dharula alichoitisha ili kutoa taarifa za ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Ujenzi wa kituo cha mabasi mkoani Njombe ulianza rasmi mwaka 2018 na kutakiwa kukamilika mapema Januari mwaka, jambo ambalo limekuwa kinyume na matarajio hayo.

Post a Comment

 
Top