0

Wabunge wa chama tawala nchini Uganda, National Resistance Movement (NRM) wamemuidhinisha Rais Yoweri Museveni kuwa Mgombea wa Urais wa chama hicho kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2021.

Hii inamaana ya kuwa, kiongozi huyo mwenye miaka 74, na aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki mwaka 1986, atagombea urais kwa muhula wa sita.

Ugombea wake katika uchaguzi ujao unakuja baada ya kusaini kuwa sheria mswada ambao uliondoa ukomo wa urais wa miaka 75. Hata hivyo, kupitishwa kwa muswada huo bungeni kuligubikwa na vurumai kubwa kutokana na kupingwa na wabunge wa upizani.

Post a Comment

 
Top