0

Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini na Mwanachama wa Yanga, Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC

Manji anadaiwa zaidi ya Tsh. Bilioni 25 ambazo ameshindwa kuzirejesha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba hivyo kusababisha mali zake zilizopo Mwanza na Dar es Salaam ambazo ziliwekwa dhamana, kuzuiwa

Mali hizo zimezuiwa kwa oda mbili tofauti za Mahakama hiyo, zinazomzuia Manji kufanya muamala wa aina yoyote kuzihusu ikiwamo kuhamisha umiliki kama zawadi, kuuza au kuweka dhamana

NBC ilifingua kesi mwaka 2016 ikizishtaki kampuni za Farm Equip (T) Limited, Tanperch Limited na Quality Group Limited zinazomilikiwa na Kaniz Manji na Yusuf Manji kwa kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15.9 bilioni.

Post a Comment

 
Top