0
Mashinji Azungumzia Kuhusu CHADEMA 'Kufa' Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amesema chama chao hakitaweza kupoteza mvuto kwa upande wa Zanzibar licha ya aliyekuwa Katibu Mkuu CUF, Maalim Seif Sharif ambaye anatajwa kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi visiwani humo.

Dkt. Mashinji ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv juu ya hatua ya Maalim Seif kuhamia ACT - Wazalendo na kukifanya chama hicho kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa visiwani Zanzibar ambapo amesema wananchi wa Zanzibar bado wanawakumbuka.

Mashinji amesema, "siasa ni mtazamo, kama wamefanikiwa kuwaaminisha wananchi kuwa itakuwa hivyo basi wamefanikiwa, lakini siasa wakati wote inabadilika wananchi wa Zanzibar waliipigia CHADEMA 2015, nina imani wananchi bado hawajasahau kuwa CHADEMA ni kipenzi chao."

Kuhusiana na ACT kujiunga UKAWA, Mashinji amesema, "kwa mazingira ya kisiasa kwa sasa tunahitaji kuungana pamoja kweli ili kuhakikisha tunapambana zaidi na CCM".

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji alimpongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Post a Comment

 
Top