0
Huyu Ndie Mtanzania Aliyeshinda Tuzo ya Malkia
Tanzania imeendelea kusikika na kuvuma katika anga za kimataifa hasa katika sekta ya elimu, hii ni baada ya mtanzania Given Edward kushinda tuzo ya Vijana ya Umoja wa Ulaya (European Youth Awards- 2018) inayowatambua vijana wanaotumia teknolojia kuleta matokeo chanya katika jamii.


Given ameshinda tuzo hiyo kupitia programu yake ya simu (App) ya Mtabe  inayowasaidia wanafunzi wa shule za sekondari kujifunza masomo ya darasani kwenye viganja vyao hata pasipo kuunganishwa na mtandao wa intaneti.

Nyota yake iling'aa zaidi mwaka 2015 alipopata tuzo ya Malkia wa Uingereza kwa viongozi vijana (The Queens Young Leaders) ambayo hutolewa kila mwaka kama njia moja ya kuitambua kazi inayofanywa na vijana katika jamii mbalimbali za mataifa ya Jumuiya ya Madola.

Ushindi huo ulitokana na App yake ya MyELimu  kufanya vizuri kama jukwaa la mtandaoni linalowaunganisha walimu na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari kukutana na kujadili masomo pamoja.

Ungana nasi kufahamu safari ya Given alikotoka na matarajio aliyonayo katika kutumia teknolojia rahisi kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. Bofya link hapo kumtazama akifunguka zaidi

Post a Comment

 
Top