Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST
linatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 21 hadi 28 mwaka huu
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Tamasha la
JAMAFEST Mwaka huu linaongozwa na Kauli mbiu “Uanuai wa Kitamaduni; Msingi wa Utengamano wa Kikanda,Maendeleo ya Kiuchumi na Kushamiri kwa Utalii.
Tamasha la JAMAFEST lilifanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda mwaka 2013 ambalo
lilihudhuriwa na washiriki17,500 Kenya ikafuatia mwaka 2015 kwa kuwa na washiriki
21,000 na Uganda mwaka 2017 ambapo washiriki 42,600
Utakumbuka Tamasha la JAMAFEST linafanyika kwa mzunguko miongoni mwa nchi wanachama wa Jumiya ya Afrika Mashariki kwa kila baada ya miaka miwili kwa mujibu wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki la mwaka 2012.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment