Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyetokea kwenye mashindano ya Bongo Star Search, Kayumba, amekiri kuwa karibu zaidi na muigizaji Irene Uwoya, lakini sio sababu ya kumtumia kupata kiki.
Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television , Kayumba amesema ni kweli yupo karibu na msanii huyo kutokana na kupenda kazi zake, na amekuwa akimsapoti sana kwenye muziki wake.
Akizungumzia hilo Kayumba amesema hata hivyo hawezi kumtumia Irene ili kupata kiki zaidi, kwani anaacha kazi zake zijitangaze zaidi, ambazo ndio zilizomfanya awe karibu naye.
Kayumba akifunguka hayo amesema hivi
“Mimi sipo kwa ajili hiyo, mimi nafanya muziki wangu, mtu ambaye anapenda muziki wangu atanisapoti, Irene Uwoya alipenda Muziki wangu akanisapoti , hakuna kitu ambacho nilikuwa nakiogopa ili kuweka hilo wazi, ila ana mchango kwenye kazi zangu, kwani lipo jambo ambalo amenisapoti, ukifika muda litaonekana”, amesema Kayumba.
Ikumbukwe kuwa tangu Irene Uwoya atalikiane na mume wake Dogo Janja, wengi wamekuwa wakitaka kujua nani yupo naye kwenye mahusiano, jambo ambalo msanii Kayumba akahusishwa naye baada ya kuonekana yupo naye karibu sana, licha ya wenyewe kuamua kufanya siri.
Post a Comment