0
 
Msanii Foby ambaye ndiye aliyemtoa kimuziki Hamisa Mobeto baada ya kumuandikia wimbo wake wa Madam Hero, amefunguka kitendo alichofanyiwa na Hamisa, ambacho anadai kimemkatisha tamaa sana.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Foby amesema kwamba baada ya kuamini kuwa Hamisa ameshatoka kimuziki, alimuomba afanye naye kazi ili ampe shavu kutokana na umaarufu wake, lakini cha kushangaza mpaka sasa Hamisa bado anamzungusha, licha ya jitihada zote alizofanya juu yake.

Akiendelea kuelezea hayo Foby amesema alipata shida sana na Hamisa kumtengeneza kimuziki kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuimba jambo ambalo ana ushahidi nalo kwani ana clip zake, na muda mwingine kutamani hata kumpiga pale alipomuona akifanya vibaya alikuwa akiimba studio.

Mwenyewe asimulia zaidi

“Kila kitu kinatokea kwa sababu, nilipanga ngoja nimuweke huyu mdada kwa sababu nishamtengeneza kimuziki, nimuweke kwenye wimbo wangu, so unajua wabongo wanapokuwa wanahitaji kitu, wanakuwa wapole, lakini wakishapata basi tena, nikamcheki akaniambia ngoja nifikirie”, amesema Foby.

Foby aliendelea kuelezea “mimi ndio nimemuweka kwenye muziki, nimemtengeneza, alikuwa sio kitu chochote, akiimba hakuna mtu anayeweza kumkubali, C9 ana clip nyingi tu kanionyesha, nikiwa naye studio nilikuwa napata hasira nusu nimpige makofi, mpaka madam hero imetoka mpaka viongozi wamekukubali, halafu unanidharau mimi, nakwambia nikuweke kwenye wimbo wangu ili YouTube yangu ichangamke, unaniambia ufikirie!!”.

Msanii huyo ambaye ni muandishi mzuri wa ngoma amesema alifanya kazi ile na Hamisa ili kumsaidia kutokana na kuwa kwenye kipindi kigumu, lakini yeye alikuwa naye bega kwa bega kuhakikisha anafanikiwa.

Post a Comment

 
Top