BAADA ya hivi karibuni kuposti picha akiwa na mpenzi mpya mbali na aliyezaa naye anayejulikana na wengi, mwigizaji anayefanya poa kunako Tasnia ya Filamu za Bongo, Yusuf Mlela amefunguka mengi.
Katika mahojiano maalum na Showbiz Xtra, kwa mara ya kwanza Mlela ameeleza maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi;
Showbiz: Siku hizi unaigiza sana tamthiliya tofauti na filamu, kwa nini?
Mlela: Unajua soko limebadilika sana, siku hizi limehamia kwenye tamthiliya. Hata pesa ipo huko. Kwa hiyo tunafanya tamthiliya ili kujikimu zaidi na kupata kiwango kikubwa cha pesa tuweze kufanya mambo mengine makubwa zaidi zikiwemo muvi, kwa sababu sasa hivi tasnia yetu ni kama imelala. Watu wanahitaji vitu vipya, ndiyo maana tunajaribu kufanya tamthiliya ili tuweze kujenga msingi wa kufanya filamu kubwa zaidi.
Showbiz: Wewe kama mkongwe katika tasnia umewahi kuwaza kuwasimamia au kuwasaidia wasanii?
Mlela: Ndiyo nimewaza kusimamia wasanii, isitoshe kuna wasanii wengi nimewasimamia na hadi leo hii wanatambulika kwa sababu ya mimi Yusuf Mlela, wapo wengi mfano Jada, Slim Omary, Nisha na wengineo. Ni wasanii ambao niliwaona na nikawatambulisha.
Hadi leo wanatambulika na bado naendelea kutambulisha wengine.
Kwa mfano sasa hivi nimefanya tamthiliya yangu inaitwa Kauli, Mungu akisaidia itatoka muda si mrefu, humo kuna wasanii wengi wachanga.
Showbiz: Kuna video umeposti ukiwa na mwanamke mwingine ndani ya mahaba mazito, hivi ndiyo yule ambaye umezaa naye au?
Mlela: (Anacheka) hapana, huyu ni mpenzi mwingine siyo yule ambaye nimezaa naye.
Showbiz: Kuna kipindi uliwahi kunukuliwa ukisema huwezi kumuoa mwanamke uliyezaa naye kwa sababu haendani na wewe na ilikuwa bahati mbaya tu mkapata mtoto, hii imekaaje?
Mlela: Hapana, sikusema kwamba hatuendani, lakini siyo lazima mkizaa muoane, mnaweza tu mkazaa na mwisho wa siku kila mtu akaendelea na mambo yake na hiyo desturi siyo ya kwangu peke yangu ipo dunia nzima.
Showbiz: Kwa hiyo unataka kusema mlizaa kwa makubaliano?
Mlela: Haikuwa kwa makubaliano, lakini naweza kusema kwamba, ilitokea tu tukawa tumepata mtoto, lakini tabia zikawa tofauti kizuri tulikuwa hatujafunga ndoa wala kujitambulisha popote hivyo ilikuwa ni ruksa kuachana.
Atabaki kuwa mzazi mwenzangu ni mtu ambaye namheshimu kwa sababu amenizalia mtoto.
Shobiz: Mtoto kwa sasa anaishi na nani?
Mlela: Mtoto nipo naye, namsomesha, yupo darasa la kwanza, ana umri wa miaka sita.
Showbiz: Vipi kuhusu kumsaidia mtoto wako kuingia kwenye sanaa ya uigizaji, ungependa iwe hivyo?
Mlela: Hapana, sitaki mtoto wangu nimuingize kwenye uigizaji, nataka yeye mwenyewe kama atapenda ndiyo baadaye aingie, lakini sitaki nimtengeneze katika mazingira haya, nataka yeye mwenyewe ndiye achague maisha yake. Pia kama atapenda sanaa, nitamruhusu.
Showbiz: Kuna kipindi ulinenepa sana, lakini sasa hivi unaonekana umepungua, nini siri ya mabadiliko yako ya kimwili?
Mlela: Kiukweli ni mazoezi kwa wingi, kwa sababu siku hizi unene siyo dili, unatakiwa uwe na kifua kizuri yaani ‘Six Pack’, hata ukivua shati unakuwa na muonekano bomba.
Nafikiri sasa hivi dunia imebadilika, mambo ya kuwa na tumbo hapana, kwa hiyo sasa hivi nimeukataa unene hivyo nitaendelea kujijali na kuwa na muonekano mzuri nikiamini nitaendelea kuwa kijana siku zote.
Shobiz: Hivi mpenzi wako wa sasa ni Mkenya au Mtanzania?
Mlela: Hahaha ni Mtanzania.
Showbiz: Vipi naye ni msanii?
Mlela: Hapana. Huyu mtu yupo tofauti kabisa na sanaa.
Showbiz: Okey, lini tutegemee ndoa?
Mlela: Kiukweli nampenda sana, lakini ndoa ni mpango wa Mwenyezi Mungu. Muda utakapofika, basi nitatimiza. Hivyo siwezi kusema ni lini, lakini hivi karibuni.
Showbiz: Neno la mwisho kwa Watanzania?
Mlela: Nawashukuru sana Watanzania kwa kunisapoti mimi kama Mlela. Ni miaka zaidi ya 13 nipo kwenye tasnia, siyo mchezo, nimehangaika sana hadi leo hii naweza kumiliki kampuni yangu. Nawaambia ahsante sana, waendelee kunisapoti na kusapoti kazi zangu. Pia kuna Tuzo za Sinema Zetu (#sziff2019), naomba Watanzania wanipigie kura kama Best Actor na jinsi ya kupiga kura ni hivi: Andika SMS 260*9 kwenda 0683520006.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment