0
Q Boy Afunguka Sababu Iliyomfanya Amlilia Daimond
Msanii Q-boy amefunguka na kutaja sababu kubwa iliyomfanya kulia siku alivyotajia jina la aliyekuwa bosi wake hapo awali na kusema kuwa sababu kubwa ni kwamba amekuwa akimkumbuka sana Diamond kwa sababu akiangalia alikotoka, alipokuwa na alipo kwa sasa anaona kabisa kuna utofauti mkuwa ambao unamfanya aumie kila siku.

Msanii  Q-boy ambae amewahi kufanya kazi chini ya lebo ya wcb amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba kwa sasa amekuwa akijitegemea, lakini kila mara amekuwa akimkumbuka sana Diamond kwa sababu ya jinsi alivyokuwa akilelewa katika lebo hiyo.

Q-Boy aliwahi kusikika akisema kuwa hata kama angekuwa tajiri kasi gani lakini bado anaona kuwa bado anamuhiaji sana bosi huyo kwa sasa katika maisha yake ya muziki.

Post a Comment

 
Top