Tetesi za MOSES Iyobo Kuikimbia WCB, Mwenyewe Afunguka Haya
Dansa maarufu kutoka WCB ambaye anafanya kazi kwa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa muda mrefu, Mose Iyobo ameibuka na kudai kuwa bosi wake huyo ni mtu poa sana.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Mose Iyobo amefunguka na kusema Bosi Wake Diamond ni mtu poa sana na ni bosi mzuri kufanya naye kazi.
Diamond ni mtu fulani ambaye yupo poa sana yaani Siwezi kusema nitoke pale (WCB) eti niende sehemu nyingine! Labda nikafungue kitu changu mwenyewe”.
Lakini pia Mose Iyobo ametupilia mbali Tetesi Za kuwa analelewa na mzazi mwenzake Aunty Ezekiel na kudai anatengeneza hela nzuri tu kama Dansa wa Diamond hivyo hahitaji kulelewa.
Nalelewaje wakati nafanya kazi kwa Diamond? Nikimwambia Diamond nataka gari Fulani yaani inachukua dakika chache tu”.
Post a Comment