Ombi la MSANII Wakazi Kwa Wasanii Wenye Pesa
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Wakazi amefunguka na kuwataka wasanii wakubwa ambao wana majina makubwa na wenye pesa wawasaidie wasanii wengien wadogo,
Wakazi amewataka wasanii kuwa na ushirikiano na kunyanyuana ambapo amesema kuwa wasanii wenye majina makubwa na pesa wawekeze kwa wasanii wachanga na wasiojiweza.
Kipitia ukurasa wake wa Instagram, Wakazi ameandika:
WAKUTUKOMBOA NI SISI WENYEWE… #Artists
Huu ni wito wangu kwa wasanii wenzangu. Wasanii Wenye majina makubwa washikeni mkono wasanii wachanga. Na Wasanii wenye hela fanyeni investment kwa Wasanii wachanga.
Ujue kuna Wasanii wana majina makubwa na wana hela, ila public interest imepungua. Wamefika kikomo cha umaarufu wa ndani. The only way they can get bigger ni kwa ku explore masoko ya nje. Sasa ukifikia hiyo level, ni bora ubadilishe jinsi unavyo attack market (focus on international one), na pia vi vyema kutoa a “helping hand” kwa upcoming Artists. Sasa hivi kujenga jina/brand hadi uwe household name ni changamoto sana regardless how talented you are. Na hakuna kitu kinauma kama kuwa Talented alafu level ya mafanikio hususan kiuchumi ni almost nothing.
Wewe kumsaidia “underground” kunaweza kukurudisha hata wewe kwenye ramani, alafu mambo yakaenda. Let’s embrace the young artists and respect their ideas cause in reality it’s them and their peers, who are the current consumers of the music.
Ila maandaglaundi na nyie Acheni kulia lia. Onyesheni THAMANI zenu kwa washika dau, Big Artists and more importantly kwa Mashabiki, badala ya kukariri tu “naomba unisaidie”. Huhitaji kuwa signed au kupata sponsor ndio uanze ku-act ki professional au kujinadi kwenye Social Media, au ku exhibit Nidhamu ya kazi, etc. (Nitalichanganua hili swala vizuri siku za karibuni). Ila kiufupi, wakati unasubiri bahati ya kushikwa Mkono na Msanii mkubwa au yeyote yule (Media, Presenter, DJ, Mashabiki), Anza kujijenga na kujijengea mazingira ya kuonekana you are worthy and worth it!!! Only We, can save ourselves !!! #Workethic ”.
Post a Comment