0

Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma, amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka sheria zote mtandaoni ili Watanzania wote wapate kuzifahamu.

Amesema hatua hiyo itawasidia Watanzania kufahamu sheria kabla ya kufungua mshahauri mahakamani na mambo mengihne yanayohusu sheria.

Jaji Mkuu amesema hayo leo Jumatano Februari 6, katika kilele cha siku ya maadhimisho ya Sheria zilizofanyikia jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais John Magufuli.

Amesema wananchi wasiwaache wanasheria wabaki peke yao, wanatakiwa kufahamu sheria hasa kwenye mirathi kabla ya kufungua shauri hilo.

“Kabla ya kuanza kesi inabidi mwananchi ahakikihse anafahamu hatua zote ambazo kesi yake itapitia.

“Huhitaji elimu ya sheria angalau kujua hatua za kuchukua katika kupata haki,” amesema Jaji Mkuu.

Pamoja na mambo mengine, amesema mfumo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), italeta mapinduzi iwapo itashirikisha wadau na wanasheria wote.

“Mfumo wa kielektroniki wa kusajili mashauri kwa njia ya kielektroniki kwa mfano kufungua sheria benki ya kuhifadhi hukumu zinazotolewa, kurahisisha wananchi kusoma hukumu zinazotolewa, mfumo wa kusajili mawakili na mfumo wa utambuzi wa kimahakama,” amesema.

Post a Comment

 
Top