Shepu FEKI Yamtoa Povu Nisha
BAADA ya kuambiwa kuwa anafeki umbo lake kutokana na kwamba kiuhalisia hayupo hivyo, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kuwatolea povu watu ambao wamekuwa wakimsema. Nisha amefikia hatua ya kutoa povu hilo baada ya hivi karibuni picha zake kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa na umbo namba nane huku nyingine akiwa hana shepu kabisa na mashabiki kuanza kumshambulia wakisema anafeki umbo.
Akichezesha taya na Risasi Jumamosi, Nisha alisema watu wamekuwa wakichonga sana hivyo amewaachia nafasi waendelee kwani hawamuongezei wala kumpunguzia chochote. “Hao mashabiki nimewaacha tu wazidi kushambulia kwa sababu bando ni lao, simu ni zao, mimi sijali chochote maana kujibishana na watu ni kupoteza muda kwenye vitu ambavyo siyo muhimu wala havina faida kwangu,” alisema Nisha.
Post a Comment