Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema hajui kama CHADEMA wamepeleka barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) FIFA baada ya kumtaja Tundu Lissu katika Mkutano Mkuu wa TFF Arusha.
Siku moja iliyopita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)wameliandikia barua kwenda FIFA kuhusu kauli iliyotolewa na Rais wa TFF dhidi ya Mwanasheria Mkuu huyo wa Chama chama hicho.
Mwisho mwa wiki iliyopitia kwenye mkutano Mkoani Arusha, Rais wa TFF alieleza kuwa atapambana na wote wanajida 'kina Tundu Lissu' kwenye soka kwa lengo la kukwamisha maendeleo.
Rais huyo wa TFF ameeleza kutokuwa na taarifa yoyote juu ya barua hiyo na akisema hajajua haswa kilichoandikwa nini ndani yake, wala hawezi kuzungumzia suala lolote juu ya CHADEMA kwenda FIFA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment