Mlinzi wa klabu ya Simba, Erasto Nyoni amehudhuria mazoezi ya klabu yake jana kwa mara ya kwanza tangu alipoumia mwezi Januari mwaka huuu na kuleta ahueni ya uwezekano wa kurejea uwanjani hivi karibuni.
Licha ya kuonekana mazoezini, lakini hakujumuishwa katika programu ya mazoezi ya mwalimu, ambapo amesema kuwa kuna uwezekano wa kurejea dimbani hivi karibuni endapo vipimo vyake vitaonesha yuko fiti.
"Napenda kuwashukuru wanachama wa Simba na mashabiki kwa sapoti yao kwetu, Mwenyezi Mungu ameweza kuniponesha mpaka sasahivi muda wowote naweza kurejea uwanjani. Kwahiyo wasikate tamaa, waendelee kuwa na sisi ili hizi mechi zinazofuata tuweze kufanya vizuri", amesema.
Aidha Erasto amezungumzia juu ya kipigo ilichoipata timu yake katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika hivi kkaribuni, ambapo amesema, "wenzetu walikuwa makini sana kwamba walikuwa makini wanapopata nafasi wanazitumia".
"Mpira ndo hivyo ulivyo, tumetokea tumefungwa kwahuyo tunajipanga tena kivingine ili tuweze kufanya vizuri mechi zinazofuata", ameongeza Nyoni.
Nyoni amekua nje ya uwanja akiuuguza majeraha aliyoyapata katika mechi za Kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwezi wa kwanza, na anatarajiwa kurudi uwanjani muda wowote kuanzia sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment