Polepole Ataka Godbless Apuuzwe
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na wananchi kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha amewataka wananchi kumpuunza mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbles Lema na timu yake ambayo imekuwa ikimkashifu rais na serikali kwenye mitandao ya kijamii na kuacha kutekeleza ahadi alizowaahidi wananchi wa wilaya hiyo.
Polepole alitoa rai hiyo hiyo jana wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya siki14 mkoani hapa ambapo pia alirudhishwa na utekelezaji wa ilani ya ujenzi wa barabara ya lami ya Arusha by Pass yenye urefu wa km 42.4 kutoka Ngaramtoni mpka Usa River.
“Tuna kila sababu ya kumpongeza rais wetu John Magufuli.Niwaombe wananchi wa wilaya ya Arusha Jiji pamoja tuunge mkono utendaji kazi wa rais Magufuli ambaye amejitoa sadaka kwa ajili ya kuwatumikia watanzania haswa wananchi wanyonge kwa mambo makubwa ya kusukuma maendeleo mbele ya nchi yetu”.Alisema azma ya serikali ya awamu ya tano ni kuhangaika na shida za wananchi kwa kuhakikisha wanapata maendeleo lakini pia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa kuwa ndiyo ahadi waliyoaahidi kwenye ilani ya CCM 2015-2020.
Akingumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata mbalimbali Jijini hapa Pole pole alizitaka ziwe zinawaalika maofisa watendaji wa kata pamoja na wataalam wa kata zao ili waweze kuileza ni kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye kata zao pamoja na kujibu kero ambazo hazijapata ufumbuzi.
Kuhusu Lema kumbeza rais kwenye mitandao ya kijamii Polepole alisema mbunge huyo ni mbunge wa kwenye mitandao na ndiyo sababu hajaweza kutekeleza ahadi yeyote kwa wananachi wake.
”Lema ni mbunge wenu lakini pia ni mkazi wa kata ya Engutoto lakini hajawahi hata kufika kwenye hosptali hii ya wilaya ambayo iko kwenye kata anayoishi kwa sababu hana mapenzi mema na ninyi”.
“Mpuuzeni mwacheni aendelee kumbeza rais kwenye mitando.Na muangalie kazi nzuri na kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili”.
Akikagua ujenzi wa hosptali ya wilaya ya Jiji la Arusha ambayo ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umeshakamilika kwa gharama ya sh milioni 535.5 Polepole alisema hosptali hiyo itakuwa mkombozi wa wanawake na watoto.
Baada ya ukaguzi huo Pole pole alikagua ujenzi wa vyumba vya maabara ya Biolojia na Kemia katika shule mpya ya sekondari ya Arusha Terati ambapo ujenzi wake umegharimu sh milioni 80.Awali mhandisi wa wakala wa barabara mkoa wa Arusha (TANROADS) Mgeni Mwanga alisema barabara hiyo yenye urefu wa km 42.4 inayojengwa na kampuni yaHanil Jiangsu Joint Venture Ltd ya Korea itagharimu sh bilioni 139.
Alisema hadi sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 80 na km 28 zimekamilika kwa kiwango cha lami la km 14.4 zimekamilika kwa lami ya awamu ya kwanza.Mhadisi Mwanga alisema fedha hizo ni mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika EAfDB .
Kwa upande wa fidia mhandisi hiyo alisema serikali imelipa fidia ya sh bilioni 24 kwa wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na barabara hiyo.
Post a Comment