Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dk. Gwajima akemea ubinafsi
Na. Atley Kuni- Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima, amewaonya na kuwatahadharisha watendaji katika ofisi hiyo kuepuka ubinafsi na kuwahimiza kufanya kazi kwa pamoja.
Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa kikao kazi kilicho wakutanisha Wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi na Maafisa wa Wizara hiyo kutoka Idara za TEHAMA pamoja na Afya, wkati wa wasilisho la mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali (GoTHOMIS).
Alisema,iliwaweze kufanikiwa lazima wafanye kazi kama timu moja bila kubaguana na kuonya, tabia ya ubinafsi sio nzuri na kama wanataka kukwama katika mipango yao watangulize ubinafsi mbele badala ya maslahi ya nchi kwanza. “Mimi sipo tayari kuona tunakwama wakati nilikula kiapo mbele ya Mhe. Rais, ni bora mniondoe lakini nitasimama katika kweli .“alisema Gwajima.
Dkt.Gwajima alisema anashangazwa na mataifa ya Ulaya kuendelea kupiga hatua kwenye maendeleo huku Watanzania tukibaki nyuma. “Lakini kikubwa ninacho kiona ni hali ya uratibu (Cordination) ndio changamoto kubwa katika utendaji wetu wa kila siku.” alibainisha Dkt.Gwajima.
Naibu Katibu Mkuu huyo, amezitaka Idara hizo kushirikiana kwa karibu hasa ikizingatiwa mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia yanahitaji uwajibikaji wa pamoja. “Natambua tunafanya kazi nzuri sana, lakini bila kuishirikisha kwa karibu idara ya TEHAMA, hatutaweza kufika tunapotaka kwenda” alisema Gwajima.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Afya wizarani hapo, Dkt. Anastazia Nswila, aliwataka wajumbe kuwa na msimamo mmoja katika maamuzi, kuacha kutegemea na kupangiwa misaada mbalimbali kutoka kwa wadau .
“Wadau wana pesa nyingi, isiwe sababu yakutupangia nini watatuletea, ni vizuri mahitaji yatoke kwetu sisi, kama ni Laptop tuwaambie ni aina gani tunataka, kama ni vifaa tiba huko kwenye kwenye vituo sisi ndio wakuamua aina gani ya vifaa vinafaa kulinga na mazingira yetu” alisisitiza Dkt. Nswila.
Kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa 3 kimetoka na maazimio matano ikiwepo, kuandaliwa mafunzo maalumu kwaajili yakuwawezesha idara mama ya masuala ya afya kuutambua mfumo, kuandaa andiko la jinsi gani Wizara hiyo inavyofanya katika mfumo huo, kila Wizara ifanye maamuzi ya kisekta ya ndani kabla yakukutana TAMISEMI na Wizara ya Afya, na mwisho kuwa na kikao cha wadau ili kuwapa muelekeo na msimamo wa Serikali.
Post a Comment