Inasadikika ya kwamba mwanadamu hutumia masaa mengi sana kulala kuliko kufanya kazi, hautakiki kubisha kwani huo ndio ukweli. Pamaja na kusadikika huko kuna mambo tumekuwa tukiyafanya na kuona kama hayana madhara yoyote lakini ukweli ni kwamba kadri tabia hizo zinavyojirudia ndipo unakuja kugundua madhara yake baadae sana.
Baadhi ya vitu ambavyo vipo katika maisha ya kila siku na watu wamekuwa wakijisahau kuyaepuka kabla ya kwenda kulala ni pamoja na ;-
1. Epuka kulala na simu yako karibu.
Wanasayansi wanasema kuwa kionzi ya simu ni hatari sana wa afya ya ubongo ya mwanadamu ingawa wengi wetu tumekuwa na tabia ya kuweka simu karibu na vichwa kabisa wakati wa kulala, unashauri kuzima simu yako na kuaa nayo pembeni kutoka na usalama wa afya yako.
2. Usivae saa ya mkononi wakati wa kulala.
Wanasayansi wanashauri kujitahidi kukumbuka kuuweka mwili wako kuwa na uhuru wakati wa kulaa, kitu chochote chenye kuufanya mwili wako kujihisi umebanwa sio kizuri, saa ya mkononi pia inaweza kuleta madhara sana kama utazoea kulala nayo.
3. Epukana na kupaka make-up nyakati za kulala.
wadada weng wamekuwa wakijisahau wanapotoka katika miznguko yao wanapata uvivu wa kusafisha uso ilihali uso unakuwa tayari umefanyiwa make-up na kuwekwa vipodozi, hii ni hatari kwa afya ya ngozi kwa sababu unapokwenda kulala mwili unatakiwa kupumzika hivyo make-up inakuwa imeziba vitundu vidogo vya hewa vinavyoapatikana usoni.
4. Usilale Ukiwa umevaa sidiria.
Tunasema kuwa hizi ni tabia ambazo zimekuwa za kawaida kwa maisha ya watu na kuona kama hakuna madhara yoyote lakini yapo, wanawake wanaovaa sidiria wakati wa kulala wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti.
Post a Comment