KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), anaumwa ugonjwa wa deko huku akimuomba Rais Dk. John Magufuli aanze kutibu ugonjwa huo.
Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Kilosa mkoani Morogoro, katika ziara yake ya kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimino ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM.
Dk. Bashiru alidai Lissu amekuwa akisema uongo katika nchi za Ulaya huku akiota siku moja atakuwa Rais wa Tanzania.
Wakati mtendaji huo wa juu wa CCM akiyasema hayo, Lissu amekuwa akiendelea na ziara yake katika nchi za Ulaya. Kwa sasa yupo Marekani akieleza kile alichodai hali ya demokrasia nchini na kupigwa kwake risasi.
Dk. Bashiru alidai dalili za ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment