0
Mbunge wa CHADEMA aliyepata ajali Morogoro ahamishiwa Muhimbili
Tayari Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari na wenzake wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Utakumbuka hapo jana kiongozi huyo na wenzake walipata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa wakitokea Jijini Dodoma kwenda Dar es Salaam kufuatia kuahirishwa kwa vikao vya Bunge.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene alileza hapo jana baada ya kutibiwa kwa dharura Morogoro ndipo watasafirishwa kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mkutano wa 14 wa Bunge La 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliahirishwa February 09, 2019 Jijini Dodoma baada ya kufanyika kwa wiki mbili. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelihutubia Bunge na taifa wakati wa kuahirisha Bunge liloanza Januari 29 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top