0
Inasikitisha Mtoto Aliyenusurika Kifo Baada ya Kukatwa Koromeo Afariki
Mtoto aliyejulikana kwa jina la Meshack Myonga mwenye umri wa miaka 4 mkazi wa Mji Mwema mkoani Njombe ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa koromeo amefariki dunia mwishoni mwa juma hili akiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya alipolazwa lwa ajili ya matibabu.


Mtoto huyo ambaye aliokotwa barabarani jirani na pori akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa koromeo Desemba 23, 2019 majira ya saa 4 asubuhi mtaa wa Mji Mwema.

Akizungumza kwenye mazishi ya mtoto huyo jana katika kijiji cha Ngalanga Mjini Njombe, mjomba wa marehemu Gisbeth Mlelwa, amesema  mtoto huyo alizidiwa kwa majeraha makali tangu alipovamiwa na watu wasiojulikana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo, Alanus Mwalongo ameonesha kusikitishwa na tukio la kifo cha mtoto huyo na kueleza kuwa jambo hilo linapaswa kupingwa na kila mmoja.

Hivi karibuni, Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Liberatus Sabas, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renata Mzinga wameanzisha zoezi la kuwasaka wahalifu wa matukio ya mauaji ya watoto ambapo walikagua mapori ya Nundu na Tanwat mkoani Njombe.

Post a Comment

 
Top