0

Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesitishwa na Naibu Spika, Tulia Ackson mjadala kuhusu mradi wa kufua umeme wa Bonde la Mto Rufiji, Stiegler's Gorge hadi hapo Serikali itakapoleta mkataba walioingia na mhandisi wa ujenzi wa mradi huo.

Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo leo, wakati wabunge wakichangia taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini.

Heche amesema kuna watu wamekuwa wakiimba kama kasuku kuhusu mradi huo bila kujua umeme wake utawaka mwaka 2027.

Kauli hiyo, ilimfanya Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM),  Ally Keisy kuomba kuhusu utaratibu na kumtaka Heche kufuta kauli yake kwa sababu hakuna kasuku bungeni, jambo ambalo Heche alilikubali.

Akiendelea kuchangia, Heche amesema Serikali imetenga Sh.700 Bilioni katika bajeti yake lakini fedha zilizokwenda ni Sh. 26 bilioni tu.

Amesema ili kukamilisha ujenzi wa bwawa hilo zinahitajika Sh. 7.1Trilioni na kwamba inahitajika miaka 10 ili kukamilika.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alisimama kwa kutumia kanuni ya  64 (1) na kusema Heche amevunja kanuni hiyo kwa kusema uongo bungeni.

Post a Comment

 
Top