Ajali mbaya imetokea usiku wa kuamkia leo Kata ya Hamugembe Manispaa ya Bukoba Mjini Mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 4 waliokuwemo katika magari hayo.
Ajali hiyo imehusisha magari aina ya Toyota Hiace T- 869 CHT na Fuso T-223 ATK ambapo yaligongana uso kwa uso na kusababisha mlipuko mkubwa wa moto kutokea katika eneo hilo.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi mara baada ya kufika katika eneo la tukio ambapo amesema kuwa mpaka sasa wameshaopoa maiti nne kutoka kwenye ajali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment