Uamuzi huo umelenga kupata idadi kubwa ya mashabiki watakaojitokeza uwanjani siku hiyo ili kuiunga mkono timu hiyo kwenye mechi hiyo ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.
"Tulishawahi kuwafunga Zamalek hapa. Tulishawahi kuwafunga Enyimba hapa lakini hilo halitowezekana kama hatutopata sapoti ya mashabiki.
"Pamoja na kufanya vibaya kwenye mechi mbili zilizopita, naamini kama tukipata ushindi kwenye mechi zinazofuata, bado tuna nafasi ya kusonga mbele.
"Tumekaa kama bodi ya klabu na kuamua kiingilio kwenye mchezo huo kiwe Shilingi 2000. Tunajua kuwa tunahitaji fedha lakini matokeo ni ya muhimu zaidi," alisema mwenyekiti wa bodi ya klabu hiyo, Mohammed Dewji.
Post a Comment