0

Niko kwenye mahusiano na binti mmoja kati ya wengi nilionao.

Kiukweli natamani huyu binti achepuke kwa mwanaume mwingine, huyu binti niko nae kwenye mahusiano zaidi ya mwaka mmoja sasa. Natamani achepuke labda huko atapata mwanaume atakaemfaa katika maisha yake.

Huyu binti ni mwema sana kwangu kiasi kwamba wema wake unageuka kua kero kwangu, mimi ndie mwanaume wake wa kwanza, nina uhakika hajawahi kutoka na mwanamume mwingine kabla yangu na baada yangu.

Nikiri kua nilitumia muda mwingi na gharama nyingi kumshawishi huyu binti kua mimi ndie mwanaume sahihi aliekua amemtunzia mwili wake hadi akakubali kuniruhusu kuchana nyavu.

Natamani achepuke maana huko aanaweza kupata mwanaume mwingine mwema kwake,kwa kweli hutu binti hastahili kua na mimi, ni mwema kiasi kwamba hadi namuonea huruma, anaomba radhi kwa makosa ambayo hakufanya au nimefanya mimi.

Nashindwa huyu binti namuachaje ili aende huko apate mtu anaestahili, namuonea huruma kwamba ameangukia sehemu isiyo salama, nina uhakika kuna watu wengine huko wanaostahili penzi na wema wa huyu binti mimi sistahili.

Post a Comment

 
Top