Waziri wa Mambo ya Ndani,Kangi Lugola amewatoa hofu watanzania kufuatia video clip zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha magaidi wa kikundi cha Alshabab wakitaja moja ya eneo linalopatikana Tanzania.
"Hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa na iko vizuri matukio yote ya kigaidi kutoka nchi jirani tuko makini nayo na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanaendelea kupata taarifa mbalimbali za kiintelligencia kwaajili ya kujipanga zaidi, tuwahakikishie wananchi wote kwa ujumla hakuna haja ya kuwa na hofu" alisema Lugola
Hata hivyo alisema kuwa Serikali imejipanga vizuri kwaajili ya kuhakikisha nhi inakuwa salama na amani.
Hivi karibuni kulitokea shambulio la wanamgambo wa Somalia walipoivamia hoteli moja mjini Nairobi Kenya, idadi ya watu waliofariki katika shambulio hilo watu 21 walifariki.
Post a Comment