Serikali ya Uganda kupitia Wizara ya Utamaduni na Sanaa imetangaza sheria mpya zenye lengo la kuwabana wasanii, ili kulinda maadili na sanaa kwa ujumla.
Sheria hizo ambazo zimetangazwa wiki iliyopita, zinaeleza kuwa msanii yeyote hawezi kwenda nje ya nchi hiyo kutumbuiza bila kibali .
Moja ya sheria mpya, ni kwamba Msanii yeyote wa muziki hatakiwi kupanda jukwaani akiwa amevaa nguo fupi au mlegezo.
Sheria nyingine, msanii hataruhusiwa kupanda jukwaani kutumbuiza akiwa ametumia kinywaji au kilevi chochote.
Mabadiliko hayo pia, yanamtaka kila msanii asajiliwe na haitaruhusiwa wimbo uachiwe bila kukaguliwa na mamlaka husika ya serikali.
Hata hivyo, mabadiliko hayo yamepelekea baadhi ya wasanii akiwemo Eddy Kenzo kuandaa mikutano ya kushinikiza sheria hizo zilegezwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment