0
TID na Mzazi Mwenzake Hali si Shwari Wagombaniana Mtoto... Mwanamke Adai Anababa Yake Ila si TID
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva khaleed Mohamed ‘TID’ na mzazi mwenzake Shekha Small wamejikuta katika vita ya maneno Baada ya kutofautiana katika suala la DNA (vinasaba) vya Mtoto wao.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wawili hao wameingia kwenye mvutano baada ya kila mmoja kutoa msimamo tofauti kuhusu unasaba wa mtoto wao huyo, ambapo TID anasema ni mtoto wake, wakati mama mtu akikanusha vikali.



Kwenye mahojiano na Gazeti hilo, Shekha ambaye kwa sasa anaishi Ujerumani, alisema kuwa  anachukizwa na namna TID anavyotangaza kuwa mtoto huyo ni wake, wakati siyo kweli.

Unajua huyu TID nahisi hayo madawa anayotumia (hajafafanua ni dawa za nini) yameshaanza kumuharibu, huyu mtoto sio wake kwa sababu nilishapima mpaka DNA na baba mzazi wa mtoto huyu ambaye makazi yake yapo hukohuko Bongo na majibu yakaonesha kwamba mtoto sio wa TID sasa kinachomfanya amng’ang’anie ni nini?”.

Kiukweli mimi ninachoomba TID amtoe kabisa huyu mtoto akilini mwake, kwa sababu kwanza mwanangu hajui hata kama ana baba anaitwa TID na tulishaondoka huko Tanzania tangu binti yangu akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi kumi… na sasa ana miaka mitatu, atakuwa ameshamsahau kabisa.”

Kwa upande wa TID alifunguka na kusema kuwa anachokifahamu na hakitabadilika akilini mwake ni kwamba Tania ni mtoto wake.

Huyu mwanamke ananishangaza sana, kwa sababu mimi ninachojua huyo mtoto ni wangu na mpaka kuondoka kwake hapa mimi ndio nilikwenda ubalozi kusaini ndio mtoto akapata Visa ya kusafiri.

Sasa simuelewi anavyosema nikae mbali na yule mtoto, isitoshe mimi nina mpaka ushahidi wa vyeti. Tania ni mwanangu na atabaki kuwa mwanangu siku zote”.

Post a Comment

 
Top