0
 Ndugu wa RC Ole Sendeka apotea kusikojulikana
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Elisante Ole Gabriel amebainisha kupotea kwa mmoja ya watumishi wa wizara hiyo anayefahamika kwa jina la Nikson Keiya ambaye alikuwa Meneja shamba la kuzalisha mitamba katika shamba la Sao hill.


Mtumishi huyo alikuwa akifanya kazi wilayani Mafinga Mkoani Iringa, amepotea tangu tarehe 15 Januari akiwa na pikipiki yenye namba ya usajili MC 214 BZZ aina ya King Lion katika misitu ya Sao hill.

Akizungumzia kupotea kwake, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Elisante Ole - Gabriel amesema, "ni taarifa za kusikitisha kwa kupotea kwa mtumishi mwenzetu na tunaomba familia yake iwe watulivu kwa sasa maana tumetoa taarifa kwa jeshi la polisi wanalishughulikia."

"Nashukuru msemaji wa familia ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka kwa kutoa ushirikiano  lakini pia namuomba aendelee kuituliza familia", amesema Elisante Ole-Gabriel.

Aidha Katibu Mkuu huyo amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa ukaribu kupotea kwa mtumshi huyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi

Post a Comment

 
Top