0
Katibu wa CCM Akamatwa na Polisi
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Kumotola Kumotola amekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani humo baada ya kuongoza maandamano ya wanachama wa chama hicho katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya akidai kuhujumiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chedema) ambao wameanza kufanya kampeni za uchaguzi za serikali za mitaa.



Mkuu wa Kituo cha Polisi Hai (OCD), Lwelwe Mpina ameagiza kukamatwa kwa Kumotola kwa kosa la kulizuia Jeshi la Polisi kuingia katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo maandamano hayo yalikuwa yaifanyika huku akifunga geti.



Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameagiza kusitishwa kwanza kwa shughuli zote za chaguzi hizo kwa vyama vyote vya CCM na Chadema hadi pale ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapotoa maelekezo mengine.



Aidha, Sabaya amewaonya wanachama hao na wananchi waliofanya maandamano huku akiwataka wafuate sheria za nchi na za uchaguzi.

Post a Comment

 
Top