Msanii wa muziki kutoka kundi la OMG, Young Lunya amefunguka kuhusu tetesi za kutoka kimapenzi na Jacqueline Wolper.
Rapper huyo amesema habari hizo hazina ukweli wowote ila zimesababishwa na ukaribu wao pamoja na umaarufu.
“Wolper ni dada ambaye ananisapoti katika muziki wangu na nilivyopata hizo taarifa sikujisikia vizuri kwa kweli, nilijisikia vibaya kwa maana tunaheshimiana sana, sijashangaa sana kwa sababu ni msanii kwa hiyo ni lazima iwe hivyo,” amesema.
Katika hatua nyingine kundi hilo limesema lipo katika mchakato wa kutoa albamu ila hilo litafanyika baada ya kutoa kazi zao kubwa ambazo wanazo kwa sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment