0
Sarah Umwambii Kitu kwa Harmonize Aonyesha Jeuri kwa Kumpatia Zawadi Hii

Penzi la Harmonize na mpenzi wake, Sarah bado ni moto, tena wa kuotea mbali.

Safari hii Sarah amemuonyesha Harmonize ni kwa namna gani anampenda kwa kumnunulia saa ya mkononi ambayo inatajwa kuwa ya gharama zaidi.

Katika ukurasa wake wa Instagram Harmonize aliweka kipande kifupi cha video kinachoonyesha saa hiyo na kumshukuru Sarah kwa zawadi kama hiyo na kuwataka wanaohitaji kujua gharama yake kuitafuta mtandaoni.

Saa aliyozawadiwa Harmonize inajukalikana kwa jina la Patek Philippe, saa hii katika mtandao inaoneka kuuzwa kati dola za Kimarekani 78,999 hadi 119,999. Sawa na kati ya Tsh. 177,948,749 hadi 270,308,693.

Post a Comment

 
Top