0

NAIROBI, KENYA: Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa NASA, Raila Odinga wamezungumza na kukubaliana kumaliza mgawanyiko uliopo na kuliunganisha taifa hilo kuwa moja

Raila Odinga amesema yeye pamoja na ndugu yake Uhuru Kenyatta wamekubaliana kuwa mgawanyiko ulikuwepo toka enzi za uhuru unaisha tangu leo

Kwa upande wa Uhuru Kenyatta amesema taifa la Kenya ni kubwa kuliko mtu yeyote, hivyo lazima viongozi waungane ili wananchi na taifa kwa ujumla liungane

Makubaliano hayo ya viongozi hao wawili yamekuja baada ya kufanya mazungumzo leo asubuhi Machi 9, 2018 katika jengo la Harambee House

Post a Comment

 
Top