Pichani mwenye tshet nyekundu ni baba yake mzazi Ommy Dimpoz ambapo Amesema mwanae huyo amemtelekeza miaka Mingi licha ya Dimpoz kusifika kwa kula bata nchi mbalimbali duniani.
Baba Dimpoz ana miaka 64 na ni dereva wa bajaji huko Tabora. Babaji amenunua mwenyewe. Wanaomjua wamesema anashindia mihogo na kachumbari !! .
Mzee Faraji Nyembo akizungumza na Globalpublishers anasema "Ni kama Wema Sepetu anavyohangaika kutafuta mtoto, siku akimpata hata kama hamsaidii chochote atamshukuru tu Mungu hivyo na mimi huwa ninamshukuru Mungu maana nimeshamleta Omary duniani.
Yeye kama mtoto, ndiye anayetakiwa kujua mzazi wake anahitaji nini, yaani ukimuuliza sasa hivi Dimpoz akupe namba yangu, utaona, atakujibu nini maana ninaamini hana.
Nimekuwa nikimpigia, lakini simu yake unaambiwa inatumika, angekuwa anaona umuhimu si angekuwa na namba maalum kwa ajili ya kuwasiliana na mimi baba yake kama mastaa wengine wanavyofanya kuwa na namba kwa ajili ya mashabiki na nyingine ya watu muhimu,” alisema na kuongeza “Mfano nikifa kama leo ni bora huyo Ommy asinizike au kuja Tabora maana watu watampiga na kwanza atasema ni nani wake amefariki dunia maana hivi niko hai hana ushirikiano,” alisema baba huyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment