Msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya, Ringtone Apoko amefunguka kwanini alitangaza nia ya kuwa katika mahusiano na Zari The Boss Lady.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha 1 on 1 cha Citizen TV kuwa Zari anamuhitaji mwanaume kama yeye ambaye anamjua Mungu, mrefu, handsome na anayejua kutabasamu.
“Halafu unajua nikimwangalia Zari because she is an entrepreneur anaweza akakuwa mama wa kanisa mzuri sana, ataleta maendeleo kwa kanisa,” amesema.
Soma Zaidi; Msanii wa Kenya ajitosa kwa Zari
Ameongeza kuwa sababu ya kuandika ujumbe katika mtandao wa Instagram ni ili watu kujua hilo na Mungu ataamua awe mke wake kwa sababu yupo single, ni mtu wa Mungu, ana hofu na Mungu, mrefu na handsome.
Siku ya wapendanao (Valentine’s Day) February 14 mwaka huu Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment