0

Kumekuwa na tetesi kadhaa zinazomuhusisha Mbongofleva Alikiba kufunga ndoa ya kimya kimya nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye website ya Ghafla, Alikiba anatarajia kufunga ndoa na mwanamke anayefahamika Kwa jina la Amina Ijumaa ya wiki hii (Machi 2). Harusi hiyo inatarajiwa kufanyika Pande za Mombasa huku ikihudhuliwa na watu wa karibu tu.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa staa huyo wa Seduce Me kufunga ndoa rasmi licha ya kuwa na watoto watatu kutoka kwa mama tofauti.
Harusi yake itahudhuliwa pia na wanasiasa wakubwa wa Kenya akiwemo Hassan Joho ambae ni mshikaji wake wa karibu.
lilOmmy.com itafuatilia kwa karibu kinachoonekana kuwa trend na tutarudi na taarifa za uhakika baada ya kuthibitisha kinachozungumziwa.

Post a Comment

 
Top