Msanii wa Bongofleva Nuh Mziwanda amekiri kushindwa kuwa na kifua cha kuficha mambo yake ya ndani na ndo maana imekuwa rahisi kwake kuandika nyimbo zinazohusiana na historia yake ya kweli.
Akiongea na eNEWZ Nuh amesema kwamba ''Si mara ya kwanza kuimba juu ya mahusiano yangu yaliyopita ukiacha wimbo wa Jike Shupa na sasa nimeimba wimbo mwingine unaoitwa 'Upofu' ambao ndani ya wimbo huo nimeimba yaliyonitokea kwa aliyekuwa mke wangu na mama mtoto wangu Nawal'', amesema.
Nuh amefunguka zaidi kuwa yeye sio msiri na hawezi kukaa na kitu ambacho kinamuumiza moyo lazima akiweke wazi ili abaki na amani lakini pia hutumia nafasi hiyo kuelimisha wale ambao wanamuangalia yeye kama mfano waweze kujifunza kitu kutoka kwake.
Mkali huyo pia amewaomba mashabiki zake kuendelea kumpatia sapoti katika mziki wake na kufuatilia nyimbo zake huku akisisitiza kwamba nyimbo zake zote ameimba historia yake ya kweli na ni mambo tu ambayo yanaweza kumtokea mtu yeyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment