0
Ikiwa leo February 24, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela, wasanii mbali mbali wameonyeshwa kuguswa na hilo lilomfika Sugu.

Wasanii wao wameguswa kutokana Sugu ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo waliyoipa heshima kubwa Bongo Flava na kuifanya kukubalika zaidi. Nikki wa Pili, Izzo Bizness, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego na Rama Dee watumia mitandao ya kijamii kuandika haya;

nikkwapili :Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini stay strong Jongwe

izzo_biznesss: Stay strong Big Brother JONGWE.

kalajeremiahs: TAY STRONG JONGWE

naytrueboytz: Stay Strong Brother Sugu

legendeeofficial: Nasikitika sana kwa hii habari kama Msanii pia kama Rafiki Wa Sugu,hii si picha nzuri!

professorjaytz :#This Too Shall Pass Mungu Sio KIZIWI wala Sio KIPOFU..

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamehukumu kifungo cha miezi mitano jela. Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli ambayo wanadaiwa kuitoa December 30, 2017 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge mkoani Mbeya.

Post a Comment

 
Top