0
Kaimu Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ameonekana katika televisheni ya taifa pamoja na maafisa wa jeshi na wa intelijensia jana na kutangaza kwamba vikosi tiifu zimefanikiwa kuzuia jaribio la mapinduzi lililofanywa na rais aliyejitangaza kuwa rais wa mpito, Juan Guaido.

Kujitokeza huko kumekuja baada ya mapambano kati ya waandmanaji na majeshi ya ulinzi ambayo yalianza mapema siku ya Jumanne baada ya Guaido kuwataka waungaji wake mkono kuanza hatua ya mwisho ya kumuondoa Maduro kutoka madarakani.

Kiongozi huyo wa upinzani alitoa wito kwa mgomo wa nchi nzima siku ya Alhamis kama ishara ya kuonesha nguvu dhidi ya Maduro.

Guaido aliiambia DW jana kuwa jeshi halimuungi tena mkono Maduro, licha ya idadi ndogo ya walioliasi jeshi, hakuna idadi kubwa ya waliondoka jeshini. Makabiliano makali yalizuka kati ya makundi karibu na kituo cha jeshi la anga cha Carlota, ambako Guaido alitangaza hatua yake hiyo ya awamu ya mwisho ya kumuondoa Maduro.

Post a Comment

 
Top