0
Wolper Afunguka yoyoni Kuhusu Jacqueline Mengi
KWA mara ya kwanza staa wa filamu kutoka Bongo Movie, Jacqueline Wolper, amemfungukia mjasiriamali ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ‘K Lynn’, kuwa anampenda na mara nyingi amekuwa akizifuata nyayo zake ili siku moja aje kuwa kama yeye au zaidi ya yeye.



Akizungumza na Za Motomoto, Wolper alisema kwamba mara nyingi amekuwa akimfuatilia K Lynn kwa sababu ni mwanamke mpambanaji, anajitambua na hana skendo kama ilivyo kwa watu maarufu wengine, hivyo tabia yake nzuri na nidhamu kwenye jamii ndio vinavyomfanya azidi kumpenda.

“Huwezi amini mimi na yule dada tunafanana majina mpaka tarehe za kuzaliwa, yeye amezaliwa Desember 6, 1978 wakati mimi nimezaliwa Desember 6, 1987, nadhani ndio maana damu zetu zimepatana, nampenda sana kwa sababu kwanza ni mwanamke anayejiheshimu sana, anajituma kupita maelezo.



“Jack angekuwa na skendo za ajabuajabu sidhani kama ningemfuatilia, anajiheshimu na anafanya mambo yake kwa akili sana ndio maana namfuatilia, hivyo kati ya watu ambao wanani-inspire namba moja ni yeye natamani siku moja na mimi nije kuwa kama yeye au nimzidi kabisa,”alisema Wolper

Post a Comment

 
Top