0
Wanawake 76 wamefariki dunia Mtwara
Jumla ya wanawake 76 wamepoteza maisha mkoani Mtwara mwaka 2018, kutokana na kukabiliwa na matatizo ya uzazi ikiwamo kumwaga damu nyingi wakati na baada ya kujifungua.


Hilo limebainishwa leo Machi 19, 2019 kwenye mkutano wa kujifunza na kufahamiana kwa wanawake wataaluma kutoka taasisi za umma na binafsi.

Mratibu wa afya ya uzazi kwa Baba, Mama na Mtoto mkoani Mtwara, Rozaria Arope, amesema vifo hivyo kwa wanawake ni kutokana na wengi wao kutofanya upimaji wa afya za uzazi.

Baadhi ya wanawake, wameeleza changamoto mbalimbali za kiafya wanazokabiliana nazo, ikiwemo suala la kutakiwa kupimwa virusi vya UKIMWI wanapohitaji vipimo vya saratani ya mlango wa kizazi, jambo ambalo linapelekea wengi wao kutofanya vipimo hivyo.

Wanawake hao wamekutanishwa na Shirika la Mlango wa Matumaini kwa Wanawake na Vijana, kwa lengo kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wanawake.

Post a Comment

 
Top