Walimu kutoka shule ya Sekondari ya Magu waliojitolea kujenga darasa baada ya ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza kuwa mara mbili ya watahiniwa kwa kidato cha nne waliomaliza wameelezea hatua ya ujenzi wa darasa waliloamua kujenga kwa kujitolea fedha katika sehemu ya mishahara yao ambalo litakagharimu zaidi ya Milioni 10.
Akielezea hatua ya ujenzi ulipofikia kwa saaa Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ambae pia ni Makamu Mkuu wa Shule Mwl.Mwandu Michael amesema kuwa hatua ya ujenzi imefikia uwekaji wa lenta ya kwanza baada ya kozi nne za tofari baada ya michango ya kwanza kukusanywa na walimu hao.
Ameongeza kuwa ujenzi wa darasa hilo ni wa tofauti kwani ni kubwa na lina urefu wa futi 40 na upana inchi 25 ukilinganisha na madarasa mengine ambayo yana futi 35.
Aidha amesema kuwa walimu hao wamejipanga kuchangia Shilingi elfu 35 kwa mwezi ambayo ni sehemu ya mishahara yao.
Akitoa wito kwa walimu na jamii kwa ujumla Mwl. Michael amesema kuwa suala la utatuzi wa changamoto za miundombinu mashuleni ni la kijamii na ni suala la maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi kwa ujumla sio suala la kumwachia Mh.Rais John Pombe Magufuli kwani suala la ujenzi sio lake bali ni la kijamii kwa kila anayeguswa.
"Niwaombe walimu wenzagu na jamii kwa ujumla tujitolee kuboresha miundombinu na kuinua taalumu kwa wanafunzi kwani suala la uboreshaji wa miundombinu sio la Mh.Rais Magufuli tu bali ni la kijamii kwa ujumla kwa sababu Rais atafika kikomo cha muda wa madarasa na miundombinu itabaki kwa upande wa jamii hivyo basi naomba tuunge mkono juhudi za Mh.Rais kwa kujitolea ili tuboresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi wetu".Alisema Mwl.Michael.
Kwa Upande wake Katibu wa Kamati wa ya ujenzi wa darasa hilo Mwl.Anthur Simkonda amesema kuwa ujenzi unaendelea vizuri kwani suala la kujitolea katika shughuli mbalimbali zikiwemo za uboreshaji wa miundombinu na kitaaluma shuleni hapo limekuwa la kawaida kwani mara nyingi hufuata ratiba yao bila kujali siku zisizo za masomo wanakuwepo shuleni.
Akifurahishwa na hatua hiyo ya ujenzi Mwanafunzi wa kidato cha tano Jenipher Kerman (HKL) amesema kuwa amefurahishwa kuwepo na kitendo cha walimu kujitolea na kuongeza kuwa amejifunza vitu vingi sana tangu afike shuleni hapo kutoka kwa Walimu na wanafunzi wenzake.
"Nimejifunza vitu vingi sana ambavyo nilikuwa sivijui kwani nimepata ushirikiano mkubwa sana toka kwa walimu na kwa wanafunzi na katika suala la ujenzi wa darasa hili litasaidia wanafunzi wengi ambao ambao watakuja kujiunga katika shule hii" Alisema Jenipher.
Katika Ujenzi wa darasa hilo ambalo liko chini ya usimamizi wa kamati ya Walimu unatarajia kuendelea wiki ijayo kwani wanasubiri mishahara na waweze kuendelea na hatua nyingine kwani mifuko ya saruji bado ipo.
Hata hivyo darasa hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kubeba jumla ya Wanafunzi themanini (80).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment