0
Wanaosambaza uzushi kuhusu Samatta waonywa
Shirikisho la soka nchini (TFF), limekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni, kuhusu nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta, kuwa amesema Taifa Stars haina nafasi ya kufuzu AFCON 2019.

TFF kupitia taarifa yake imeeleza kuwa taarifa hizo si za kweli na ni za uzushi huku ikisisitiza kuwa nyota huyo hajafanya mazungumzo na chombo chochote cha habari.

''Samatta hajaongelea mchezo wa Jumapili popote pale, zaidi tu anasisitiza mshkamano, kabla, wakati na baada ya mchezo'', imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa imeeleza kuwa Samatta amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani siku ya mchezo kwaajili ya kuipa nguvu timu dhidi ya Uganda ambao ni wa mwisho Kundi D.

Taifa Stars itakuwa inasaka nafasi ya kushiriki fainali za AFCON kwa mara ya pili baada ya mwaka 1980, endapo itaifunga Uganda na kufikisha pointi 8 kwenye kundi hilo linaloongozwa na Uganda wenye pointi 13.

Post a Comment

 
Top