Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin ametangaza utaratibu mpya uliowekwa na halmashauri yake katika mzunguko wa magari ya abiria yaani daladala ambao utaanza kutumika siku za karibuni.
Akizungumza jana Machi 20 na waandishi wa habari ,Kunambi amezitaja barabara hizo kuwa ni pamoja na barabara ya Kutoka mnada mpya kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba umbali wa km 42.5 nauli ni Tsh.700,Veyula kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba umbali wa km 42 nauli Tsh.750.
Barabara zingine ni barabara ya St.Gemma kwenda mji wa serikali kupitia Sabasaba km 39 nauli Tsh.700,barabara ya Swaswa kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba umbali wa km 32 nauli Tsh.600,barabara ya Mkonze kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba umbali wa km 35 nauli Tsh.650,barabara ya Benjamin Mkapa kwenda mji wa Serikali kupitia sabasaba umbali wa km 29 nauli Tsh.600.
Barabara zingine ni Udom/Utumishi kwenda mji wa serikali kupitia Sabasaba km 35 nauli Tsh.650,barabara ya Udom/Utumishi kwenda mji wa serikali kupitia Iyumbu km 16 nauli Tsh.450,na mzunguko wa ndani wa mji wa serikali nauli ni Tsh.400.
Hata hivyo Kunambi amezungumzia jitihada ambazo jiji linafanya kuhakikisha linajenga miundombinu rafiki katika mji wa Serikali kwa kushirikiana na TARURA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment